Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabiani Massawe
WAHAMIAJI
haramu zaidi ya 2,000 wameondoka mkoani Kagera na kurudi kwao nchini Rwanda
tangu
Rais Jakaya Kikwete, atoe siku 14 kwa wahamiaji kuondoka nchini kwa hiari ndani
ya kipindi hicho.
Rais
Kikwete alitoa agizo hilo akiwa kwenye ziara ya
kikazi mkoani Kagera, ambapo agizo hilo
lilihusu mkoa huo pamoja na Geita na Kigoma. Mbali na wahamiaji haramu, Rais
Kikwete aliwataka watu wanaomiliki silaha kujisalimisha kwa hiari yao kabla ya msako mkali
kuanza.
Takwimu za kuondoka kwa wahamiaji haramu zaidi ya 2,000 mkoani Kagera,
zilitolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Mstaafu, Fabiani Massawe, wakati
akizungumzia maandalizi ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu baada ya
kumalizika kwa siku 14 alizotoa Rais Kikwete.
Massawe alisema hadi sasa taarifa
ambazo wamekusanya kuhusiana na wahamiaji haramu wanaondoka kwa hiari yao kwa upande wa Rwanda wamefi kia zaidi ya watu
2,000.Hata hivyo alisema takwimu kutoka nchi nyingine bado hazijafahamika
kutokana na wahamiaji hao kupita njia za mkato.”
Takwimu za Wahamiaji
wa nchi nyingine hazijapatikana lakini wameondoka kwa kiasi chake kupitia njia
za
panya,” alisema.
Katika hatua nyingine, Massawe alisema operesheni ya kuwaondoa
wahamiaji haramu itaanza
wakati wowote kuanzia leo, baada ya kumalizika kwa siku 14 zilizotolewa na
rais.
Aliwataka wananchi mkoani Kagera kutoa ushirikiano wakati wa operesheni
kwa kuwafi chua wahamiaji haramu na watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.
Alisema ushirikiano wa wananchi ndio utakaosaidia kufanikisha operesheni hiyo
ambayo itangazwa na Rais Kikwete katika mikoa mitatu ambayo ni Kagera, Geita na
Kigoma.
“Operesheni
iko pale pale na muda wowote itaanza, baada ya muda waliopewa kukamilika, hivyo
ndugu zangu wananchi wa Mkoa wa Kagera tuwe wazalendo kuwafichua wahamiaji haramu,”
alisema.
Alifafanua kuwa watakaokamatwa wakati wa operesheni hiyo hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao
ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Kagera kutoa
taarifa za wahamiaji haramu na watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria ambazo
zinaweza kusababisha madhara makubwa miongoni mwa wananchi na taifa kwa
ujumla.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment