Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za Mafunzo Maalumu ya Ualimu Tarajali Ngazi ya Stashahada (Diploma) katika masomo ya Sayansi na Hisabati kupitia Mpango Maalumu (Bridging Course) kwa mwaka wa masomo 2013/2014. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wahitimu wa Kidato cha Sita wa Masomo ya Sayansi na Hisabati wenye ufaulu usiopungua ‘Subsidiary pass’ tatu (SSS) ili waweze kumudu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu.

Mafunzo haya yatafanyika kwa utaratibu ufuatao:

(i) Watakaochaguliwa kujiunga na Mpango huu Maalumu watapatiwa mafunzo ya miezi mitatu ya kuimarisha kiwango cha uelewa wa masomo ya Sayansi na Hisabati waliyosoma katika Kidato cha Tano na cha Sita.

(ii)  Baada ya mafunzo ya miezi mitatu, kutakuwa na Mtihani utakaopima uelewa kulingana na vigezo vitakavyowekwa. Watakaofaulu wataendelea na Stashahada (Diploma) ya Ualimu kuanzia Januari, 2014.

SIFA ZA WAOMBAJI


Waombaji wawe wamehitimu Kidato cha Sita kati ya mwaka 2000 na 2013 na kufaulu kwa kiwango kisichopungua ‘Subsidiary pass’ tatu katika tahasusi (combinations) za PCB, PCM, PGM, CBG, CBA na CBN.

MAELEKEZO MUHIMU

(i)  Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume maombi yao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa njia ya barua yakionesha anuani zao (za posta, au anuani ya barua pepe na simu), pamoja na nakala za vyeti vya ufaulu wa Kidato cha 4 na cha 6;

(ii)   Majina ya watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo haya yatatolewa mwishoni mwa mwezi Agosti, 2013 kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz na OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz;

(iii)   Barua za kujiunga na mafunzo zitatolewa na vyuo husika kwa kutumia anuani zao; na

(iv)   Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz, na OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na Vyuo vya Ualimu.

Tanbihi: Waliopo Dar es Salaam na Mikoa ya jirani wanaweza kufika Wizarani na kuweka barua za maombi kwenye sanduku lililowekwa mapokezi.

MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 20/08/2013.

 Maombi yatumwe kwa:

KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM   
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top