JESHI la Polisi nchini limewaomba wananchi wenye wasiwasi kuhusu magari wanayotaka kuyanunua kufika makao makuu ya jeshi hilo kuhakikisha kama si ya wizi na kama hayajahusika katika matukio ya uhalifu.

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, (DCI) Robert Manumba alisema kuwa kitengo cha Jeshi la Polisi Kimataifa (INTERPOL) cha jeshi hilo, kina idadi na taarifa ya magari yaliyoibwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, hivyo kina uwezo wa kumtahadharisha mnunuzi na ununuzi usio sahihi.

Aidha, alisema kuna haja kwa wanunuzi wa magari kuwa makini wakati wanapoyanunua magari hayo kwa 
Jkuwa wauzaji wengine wamekuwa na tabia ya kuuza magari yao na kukimbilia polisi kushitaki kuwa yameibwa ili walipwe na kampuni za bima.

Kuhusu wauzaji wanaodanganya wameyapoteza au kwamba magari yao yameibwa, Manumba alisema wanakuwa wakifahamu kuwa atakayepata matatizo ni mnunuzi hivyo mnunuzi huyo ndiye anayetakiwa kuwa makini na kutafuta ukweli kuhusu gari husika kabla ya kulilipia.

"Tulikagua magari 3,348 na kugundua kuwa magari 32 yalikuwa na makosa ambapo 10 kati ya hayo yalichezewa namba za chesisi, 22 yaliibwa kutoka Japan, Afrika Kusini, Uingereza, Malaysia na nchini na kulikuwa na pikipiki moja iliyoporwa hapa Tanzania," alisema hayo alipokuwa akitoa matokeo ya operesheni ya kuzuia uhalifu uliovuka mipaka, iliyofanyika nchini kwa siku tatu mfululizo kuanzia Julai 16 na kupewa jina 'Operesheni Usalama'. Alisema, walifanikiwa kukamata vielelezo na watuhumiwa wa makosa mbalimbali 61.

Chanzo: talkbongo
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top