Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein mwinyi
Serikali imesema matibabu ya saratani
kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania bado ni tatizo kutokana na kukabiliwa
na uhaba wa vifaa, wataalamu na wagonjwa
kuchelewa kufika hospitalini kwa matibabu.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa
tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dokta, Magreth Mhando wakati wa
uzinduzi wa wodi mpya ya saratani ya watoto iliyopo katika hospitali ya taifa
ya Muhimbili kwa ufadhili wa Rotary Club International.
Dokta Mhando amesisitizia kuwa
serikali itashirikiana na taasisi hizo katika masuala ya afya hususani ugonjwa
wa saratani ambao umesababisha watanzania wengi kupoteza maisha.
Naye kaimu mwenyekiti wa klabu ya ROTARY SHARMILA BHATT ambao ndio wadhamini wakuu wa
mradi huo, amesema wameamua kujenga wodi hiyo kwa lengo la kuisaidia taasisi ya
saratani ya Ocean Road ambayo imeonekana kuzidiwa na wagonjwa.
Tafiti zinaonesha kuwa ugonjwa wa
saratani kwa watoto unazidi kuongezeka katika nchi mbalimbali barani Afrika,
mfano wa saratani hizo ni saratani ya uvimbe wa uso, Saratani ya macho, na
saratani ya damu.
0 comments:
Post a Comment