Waziri Mkuu wa Libya,Ali Zeidan ametishia kutumia
nguvu kuwazuia walinzi katika bandari kuu nchini humo dhidi ya kuuza
mafuta kwa mashirika ya kibinafsi.
Afisa huyo amesema meli yeyote itakayotia nanga
katika bandari za Libya bila idhini ya serikali itashambuliwa kwa
bomu.
Wafanyakazi wa badari wamekua kwenye mgomo wiki kadhaa sasa
kulalamikia malipo ambapo maafisa wamesema mgomo huo umesababisha kupungua kwa
mauzo ya mafuta nchini Libya na hivyo kuathiri vibaya uchumi wa nchi.
Waziri Mkuu amesema serikali itatumia nguvu
zozote zile kuzuia kile amesema kuvuruga biashara ya mafuta. Banadari
zilizoathirika na mgomo ni pamoja na Zeitunia, Brega, Ras Lanouf na
Sedra. Uzalishaji wa mafuta Libya ulipungua hadi mapipa laki sita kutoka
mapipa milioni moja baada ya kuzuka mapinduzi dhidi ya kiongozi wa
zamani Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Chanzo: BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment