Shakil Afridi
Maafisa wa serikali ya Pakistan, wamefutilia mbali
hukumu ya kifungo gerezani aliyopewa daktari aliyewasaidia maafisa wa
ujasusi wa Marekani CIA kumsaka Osama Bin Laden.
Ripoti zinasema serikali imeagiza kesi hiyo dhidi ya Shakil Afridi kusikilizwa upya.
Shakil
Afridi, alishtakiwa kwa kosa la uhaini na kufunguliwa mashtaka chini ya
sheria za kiukoo kwa kuendesha shughuli bandia ya kutoa chanjo kwa
watoto ili kukusanya habari.
Daktari huyo alihukumiwa kifungo cha miaka
thelathini gerezani mwaka 2012 ambapo tangu wakati huo amekuwa akizuliwa
katika gereza moja mjini Peshawar.
Bin Laden, aliuawa na wanajeshi wa Marekani mwezi Mei mwaka 2011 katika eneo la Abbottabad nchini Pakistan.
Kuuawa kwa Bin Laden, kulisababisha mzozo mkali
wa kidiplomasia kati ya Marekani na Pakistan ambayo ilidai operesheni
hiyo ilikiuka uhuru wake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment