CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
kimeisambaratisha ngome ya CHADEMA mjini hapa baada ya wanachama wake
365 wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa
Baraza Kuu la Vijana la chama hicho (BAVICHA), Frank Fumpa.
Wanachama hao walipokewa na Mwenyekiti
wa Umoja wa Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ,
Abdallah Bulembo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Nzovwe Sokoni
mjini hapa.
Wengine waliohamia CCM na kurejesha kadi
zao kwa Bulembo wakati wa mkutano huo ni wapiga debe maarufu wa chama
hicho mjini hapa, Alex Mwaisango na Ambundwile Mwantondo.
Wanachama hao wa CHADEMA waliohamia CCM
wakati wa mkutano huo na kupokewa na Bulembo ni miongoni mwa wanachama
375 kutoka vyama vya upinzani wakiwemo wanne kutoka CUF na sita kutoka
TLP.
Katika mkutano huo pia Bulembo
alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa CCM 279 wakiwemo vijana 15
waendesha pikipiki (Bodaboda), Umoja wa Wazazi Tanzania 15 na Umoja wa
Vijana wa CCM (UVCCM) wanachama 15.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake sababu
za kuodoka CHADEMA na kuhamia CCM, Fumpa alisema baada ya kutafakari kwa
kina kwa muda mrefu walipokuwa ndani ya chama hicho wamegundua hakina
mpango wa kuwatetea na kuwaletea maendeleo Watanzania zaidi ya
kupanikiza chuki na uhasaba kwa wananchi dhidi ya serikali yao.
Fumpa alisema wakiwa ndani ya chama
hicho wameshuhudia mengi ikiwemo msimamo wa viongozi wa chama hicho wa
kuwatumia wanachama hususan vijana wa chama hicho kuongoza vurugu na
kutokana na vurugu hizo katika baadhi ya maeneo zimesababisha vifo vya
watu wasio na hatia.
Alisema wameamua kurejea CCM kwa umamuzi
wao bila kushawishiwa na yeyote baada ya kubaini wanapoteza muda mure
wa kushiriiana na Watanzania wengine kuharakisha maendeleo yao na
kuwashauri warejee CCM kwenye matumaini ya kweli ya ufumbuzi wa
changamoto zinazowakabili.
"Zipo kauli za baadhi ya viongozi wa
vyama vya upinzani wanapowaona wenzao wameamua kurudi nyumbani CCM kuwa
wamenunuliwa au kuahidiwa vitu fulani, tuwahakikishie wananchi wenzetu
kuwa tumeamua kurejea kwa baba na mama kwa hiari yetu bila kushawishiwa
nanyi njooni nyumbani tujenge taifa letu", alisema Fumpa.
Akihutubia mkutano huo, Bulembo
aliwataka wananchi wa Jimbo la Mbeya mjini kujutia uamuzi wao
waliouchukua mwaka 2010 wa kumchaguae Joseph Mbilinyi 'Sugu'wa CHADEMA
kuwa Mbunge wao kwa kutorudia kosa hilo katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
"Ndugu zangu kufanya kosa si kosa kosa
ni kurudia kosa, mwaka 2010 mlimchagua Sugu wa CHADEMA kuwa Mbunge wenu,
lakini hawasaidii kuleta maendeleo yenu zaidi ya kuipinga serikali ya
CCM kuleta maendeleo, hivyo msirudie kosa hilo katika uchaguzi wa
serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2015", alisema Bulembo.
Bulembo aliyeko katika ziara ya kukagua,
kuhimiza uhai wa Chama na jumuia zake, kukagua utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM mkoani hapa alisema kuchagua upinzani ni kuthoofisha
jitihada za serikali ya CCM ya kuharakisha maendeleo yao.
Alisema vyama vya upinzani kikiwemo
CHADEMA haitakii mema CCM na vimekuwa vikifanya kila liwezekanalo
kuhakikisha ilani ya CCM inayolenga kuondoa kero na changamoto
zinazowakabili wananchi haitekelezwi, hivyo kuchagua upinzani ni sawa na
kusitisha kwa muda maendeleo yao.
Via Ccmblog
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment