Askari polisi wa Wilaya ya Hai wakiandaA mwili wa mfanyabiashara wa
madini Erasito Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la
Wasomali, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuupeleka chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospitali ya wilaya hiyo.
Mfanyabiashara tajiri wa Mirerani na Jijini Arusha, Erasto
Msuya, ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 kwa kutumia bunduki aina
ya Sub Machine Gun (SMG), jana mchana.
Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri, aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
“Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya
risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa
kweli ameuawa kinyama sana,” alisema polisi mmoja wa Kituo cha
Bomang’ombe.
Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomang’ombe,
mji huo ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na
Mererani.
Habari za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake
walikuwa katika pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo, walimpora
kibegi ambacho haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya
fedha.
Kulingana na vyanzo vya habari, mfanyabiashara
huyo alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa
Bomang’ombe na makutano ya Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai
kwenda Arusha.
RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa saa 7:00 mchana eneo la
Mjohoroni kati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya barabara ya Kia.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eransto
alikuwa akitokea Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la
Mjohoroni alichepuka na kwenda meta 300 nje ya barabara,” alisema.
Kamanda Boaz alisema alipofika eneo hilo,
alikutana na vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani
ya gari kwa lengo la kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.
Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye
gari lake na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka
kwenye gari la Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi.
Pikipiki iliyotumika yapatikana
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Kijana wa Kimasai alivyoshuhudia mauaji
Kijana pekee wa kabila la kimasai anayedaiwa
kushuhudia mauaji hayo, aliwaeleza polisi kuwa mara baada ya Erasto
kufika eneo hilo la mtaa wa Wasomali, alisimamisha gari na kuwapigia
wauaji.
Habari hizo zimedai kuwa vijana wale wawili
walipokea simu hiyo na kumtaka ashuke kwenye gari lake la kifahari aina
ya Range Rover New Model, ili wafanye biashara ambayo haijui.
Inadaiwa kuwa Erasto alipojaribu kupeleka mkono
ili achomoe bastola, mmoja wa wale vijana alianza kumshambulia kwa
risasi nyingi ambazo zilimfanya afariki dunia papo hapo.
Kijana huyo wa kimasai anayedaiwa kuwa msaada
mkubwa kwa polisi, alidai kuwa baada ya Erasto kudondoka chini, vijana
hao walichukua begi alilokuwa nalo na kutokomea.
Pikipiki iliyotumika yapatikana
Taarifa zilizopatikana baadaye jana jioni zilisema
pikipiki iliyotumika katika tukio hilo imepatikana katika kijiji cha
Olkolili, huko Sanyajuu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.
Kamanda Boaz alithibitisha kupatikana kwa pikipiki
hiyo yenye nambari za usajili T316 CLV ikiwa imetelekezwa baada ya
gurudumu moja kupata pancha baada ya kufika katika eneo hilo.
“Kwa vile tulikuwa tumesambaza taarifa kila mahali kuna raia wema walituarifu kuwa kuna watu wametelekeza pikipiki,
baada ya kupata pancha na walikuwa wakitembea kwa miguu,” alisema.
Alisema Polisi walikwenda katika eneo hilo na
mashuhuda walioshuhudia tukio hilo la mauaji wameitambua pikipiki hiyo
kuwa ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na wauaji wa mfanyabiashara huyo.
Kamanda Boaz alisema pia kuwa polisi watachunguza
kwa kina mawasiliano ya simu ya mfanyabiashara huyo, kwa lengo la
kutafuta watu wa mwisho kuwasiliana na marehemu.
Utajiri wake marehemu Msuya
Katika kipindi cha uhai wake, marehemu alikuwa akijihusisha na uchimbaji na biashara ya madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani na jiji la Arusha.
Kutokana na biashara zake hizo, alimudu kumiliki mali kadhaa zikiwemo
Kutokana na biashara zake hizo, alimudu kumiliki mali kadhaa zikiwemo
nyumba za kawaida za kuishi pamoja na hoteli maarufu Arusha ya SG Resort iliyoko eneo la Sakina.
Pamoja na hoteli na nyumba kadhaa zilizoko mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, marehemu pia alikuwa akimiliki magari kadhaa ya kifahari. Nyongeza na Peter Saramba, Arusha
Via Mwananchi
0 comments:
Post a Comment