Serikali imetoa waraka namba 1 wa mwaka 2013 ambao unamtaka kila mwanafunzi au mwanachuo kuchangia kiasi cha shilingi 1000 kwa mwaka na fedha hizo zitatumika katika ukaguzi wa shule au vyuo ambapo imeelezwa kuwa ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Ada hiyo ni tofauti na ada ya awali ambapo kila mwanafunzi wa sekondari na wa chuo amekuwa akichangia shilingi 500/= wakati wanafunzi wa shule za msingi wamekuwa wakichangia shilingi 200 kwa mwaka tangu mwaka 1998.

Waraka huu unafuta Waraka wa Elimu wa mwaka 1999 na unaanza kutumika kuanzia Januari 2013.
 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top