Licha ya kuongezwa kwa ulinzi, bado matukio ya mauaji yameendelea kushamiri mashuleni.
Wanafunzi 29 na
mwalimu mmoja wameuawa baada ya Waislamu wenye msimamo mkali kuvamia
shule ya bweni kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Walionusurika,
ambao wamekuwa wakitibiwa majeraha ya moto na risasi, wamesema baadhi
ya wanafunzi walichomwa moto wakiwa hai katika shambulio hilo jana
kwenye Shule ya Sekondari ya Serikali mjini Mamudo katika jimbo la Yobe.
Mkulima Malam Abdullahi alilia juu ya miili ya watoto wake wawili wa kiume, wenye umri wa miaka 10 na 12.
"Hivyo ndivyo ilivyo, ninawahamisha watoto wangu wengine wa kiume kutoka kwenye shule hii," alieleza Malam. Alisema alikuwa na watoto wengine wadogo watatu kwenye shule moja ya jirani na hapo.
Alisema
hakukuwa na ulinzi kwa wanafunzi licha ya kuwapo maelfu ya wanajeshi
tangu serikali ilipotangaza hali ya hatari katikati ya Mei kwenye
majimbo matatu ya kaskazini-mashariki.
"Tulikuwa tumelala ndipo tukasikia milio ya risasi.Nilipoamka, mtu mmoja alikuwa kanielekezea mtutu wa bunduki," alisema Musa Hassan mwenye umri wa miaka 15.
Aliinua
mikono yake juu kujilinda, na kujeruhiwa kwa risasi zilizolipua vidole
vyake vyote vinne kwenye mkono wake wa kulia, vile anavyovitumia wakati
wa kuandika.
Alisema
watu hao wenye bunduki walikuja na mapipa yaliyojaa mafuta ambayo
walitumia kuchoma moto jengo la utawala la shule hiyo na hosteli
mojawapo.
Dazeni
kadhaa za shule zimechomwa moto na idadi isiyofahamika ya wanafunzi
wameuawa kati yao zaidi ya waathirika 1,600 wakiuawa na Waislamu wenye
msimamo mkali tangu mwaka 2010.
Washambulizi
hao wamechoma majengo na kufyatulia risasi wanafunzi wakati wakijaribu
kujisalimisha, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. Wanafunzi
kadhaa wamekuwa wakitibiwa majeraha ya moto, aliongeza.
Yalikuwa
matukio matatu mabaya zaidi kuwahi kutokea kwenye shule tangu majeshi
yalipoanzisha ulinzi Mei kujaribu kupambana na Boko Haram, kundi la
harakati za Waislamu wenye msimamo mkali ambao jina lao linatafsiriwa
kama 'Elimu ya Kimagharibi ni haramu' katika lugha ya Hausa eneo la
kaskazini.
Potiskum
ipo katika jimbo la Yobe, moja kati ya tatu zilizowekwa katika hali ya
hatari iliyotangazwa na Rais Goodluck Jonathan mwezi Mei, pale
alipoamuru vikosi zaidi kwenda kwenye eneo hilo kujaribu kutokomeza
kundi hilo linaoonekana kama tishio kubwa zaidi kwa ulinzi wa taifa hilo
linaloongoza kwa kuzalisha mafuta barani Afrika.
Wanamgambo
wanaodhaniwa kuwa wa Kiislamu walimimina risasi kwenye shule moja
katika mji ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria wa Maiduguri mwezi
uliopita na kuua wanafunzi tisa, na shambulio linalofanana na hilo
kwenye shule moja iliyoko katika mji wa Damaturu lililoua wanafunzi saba
siku chache tu kabla.
Vikosi
vya Nigeria vimesema uhalifu wao umewawezesha kurejesha udhibiti wa
eneo hilo lisilofikika kwa urahisi la kaskazini mashariki kutoka kwa
Boko Haram, wakisambaratisha maeneo muhimu na kukamata wengi wa
watuhumiwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment