Mamia ya wafuasi wa kiongozi aliyepinduliwa Misri
Mohamed Morsi wamepambana na vikosi vya usalama katikati mwa mji wa
Cairo na kuwafyatulia waandamanaji hao gesi ya kutoa machozi.
Mapigano hayo yanajiri muda mfupi baada ya
mjumbe mkuu wa Marekani William Burns kutoa wito kwa vikosi vya usalama
kujizuia kwa kiwango kikubwa katika kukabiliana na maandamano hayo.
Makabiliano yalifanyika baada ya
naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayezuru Misri, kuwataka
maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutuliza ghasia wakati
wakijizuia kufanya mauaji yoyote.
Burns alikutana na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na majeshi.
Lakini chama cha Muslim Brotherhood kimesema haikina nia ya kukutana na waziri huyo.
Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa
serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi nchini, mjumbe huyo, William
Burns, amesema Misri imepewa nafasi ya pili kufuatia kupinduliwa na
jeshi Mohammed Morsi.
Alikutana na serikali inayoungwa mkono na jeshi
nchini lakini Muslim Brotherhood, inasema haina mpango wa kukutana naye.
Naibu rais wa tawi la kisiasa la chama cha Morsi, Muslim
Brotherhood,Essam el-Erian, ametoa wito wa utulivu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment