Virusi vya HIV hujificha kwenye Uboho (Bone Marrow)
Wagonjwa wawili wameondolewa bughdha ya kutumia
madawa ya kupunguza makali ya ukimwi maishani mwao baada ya kufanyiwa
upasuaji na kupandikiziwa uboho wa binadamu au (Bone marrow), hatua
inayosemekana kuondoa virusi vya HIV mwilini mwao.
Mgonjwa mmoja amesemekana kukaa kwa miezi minne
bila ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi bila ya dalili ya
kurejea kwa uogonjwa huo.
Matojeo ya utafiti huo yaliwasilishwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu maswala ya Ukimwi.
Ni vigumu sana kutibu Ukimwi, kwa sababu
hujificha ndani ya DNA, ya mtu na hivyo kusababisha virusi sugu ambavyo
haziwezi kutibika.
Madawa ya kupunguza makali ya virusi vya HIV
hudhibiti virusi hivyo ndani ya damu lakini wakati mtu anapokosa kumeza
dawa hizo, virusi hurejea.
HIV imeangamizwa?
Wanaume hao ambao hawajatajwa majina yao, wameishi na virusi hivyo kwa takriban miaka 30.
Wote walikuwa wanaugua aina ya saratani, aina ya lymphoma, ambayo ilihitaji wafanyiwe upasuaji.
Sehemu ya Uboho au Bone marrow ndipo seli mpya za damu hutengezwa mwilini na inaaminika kuwa kitovu cha virusi vya HIV mwilini.
Baada ya kufanyiwa upasuaji, hapakuwa na virusi
mwilini kwa miaka miwili kwa mgonjwa mmoja wakati mwingine aliishi kwa
miaka minne bila ya virusi kuonekana.
Ni mapema mno kuona upasuaji huo kama tiba ya
ukiwmi na hata ikiwa itasemekana kuwa tiba basi sio tiba nzuri. Ni ghali
mno na kwa baadhi ya wagonjwa kuna uwezekano wa kufariki ikiwa kwa
asilimia 15 hadi 20% kwa miaka ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji.
Wagonjwa hao sasa hawatumii tena dawa za
kupunguza makali ya ukimwi. Upasuaji huu ulifanyiwa wagonjwa hao kwa
sababu waikuwa wanaugua saratani iliyohitaji matibabu.
Mgonjwa mmoja amesemekana kukaa kwa miezi minne
bila ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi bila ya dalili ya
kurejea kwa ugonjwa huo.
Hata hivyo, madaktari waliofanya utafiti huo katika
hospitali ya matibabu kwa wanawake ya Brigham nchini Marekani, wametahadharisha kuwa
ni mapema mno kuzungumzia uwezekano wa kutibu virusi hivyo kwani
vinaweza kurejea wakati wowote.
Matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu maswala ya Ukimwi.
Ni vigumu sana kutibu Ukimwi, kwa sababu virusi
hujifificha ndani ya DNA, ya mtu na hivyo kusababisha virusi sugu ambavyo
haviwezi kutibika.
Madawa ya kupunguza makali ya virusi vya HIV
hudhibiti virusi hivyo ndani ya damu lakini wakati mtu anapokosa kumeza
dawa hizo, virusi hurejea.
BBCSWAHILI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment