Mwaka jana ni visa 64,000 vya ubakaji vilivyoripotiwa.

Mwanamume anayetuhumiwa kuwa mbakaji sugu nchini Afrika Kusini, Sifiso Makhubo, amepatikana akiwa amefariki katika chumba chake gerezani.

Sifiso Makhubo, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 122 ikiwemo mauaji na ubakaji alipatikana akiwa amejinyonga kwa blanketi.
Baadhi ya makosa aliyoshtakiwa nayo ni pamoja na kuwaambukiza waathiriwa virusi vya HIV.

Afrika Kusini ina moja ya visa vingi zaidi vya ubakaji duniani, huku polisi wakionyesha kuwa ni visa 64,000 pekee ambavyo viliripotiwa mwaka jana.

Maafisa wanasema kuwa alikuwa peke yake katika seli yake , lakini wanachunguza kilichosababisha kifo chake.

Bwana Makhubo anatuhumiwa kwa kuwabaka watoto 35 na wanawake wawili, kati ya Januari mwaka 2006 na Februari 2011.
Hadi sasa uchunguzi uliofanywa wa DNA katika waathiriwa waliodai kubakwa naye, ulithibitisha kuwa yeye ndiye alikuwa mbakaji.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top