Mfalume
Mswati III wa Swaziland akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi Rasmi wa
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba, Jijini
Dares Salaam(Kushoto kwa King Mswati III) ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda.
Mfalume
Mswati III wa Swaziland(katikati) akiwa amesimama na Meza Kuu wakiimba
Wimbo wa Taifa la Swaziland leo katika Uzinduzi wa Maonesho ya Biashara
ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam(wa pili kulia)ni Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda.
Mfalme
Mswati III wa Swaziland akiingia katika Viwanja vya Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa tayari kwa Uzinduzi Rasmi akiwa ameongozana na
Mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda.
Picha zote na Lucas Mboje wa
Jeshi la Magereza.
Mfalme Mswati wa III wa Swaziland amefungua
rasmi maonesho ya kimataifa ya biashara
katika viwanja vya mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mfalme huyo amepata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali katika
maonesho hayo ya 37 ambayo yalianza Ijumaa ya wiki iliyopita na yanataraji
kufikia tamati Julai nane mwaka huu.
Mfalme Mswati III pia alihudhuria mkutano wa
kimataifa wa manufaa kwa wote uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI



0 comments:
Post a Comment