Jeshi la
wananchi JWTZ limesema kuwa linasubiri
kibali kutoka kwa umoja wa mataifa ili kujibu mapigo kwa waasi waliofanya
shambulizi dhidi ya kikosi cha UN na kuua wanajeshi saba watanzania huku
wakiwajeruhi wengine kadhaa.
KANALI
kapambale Mgawe amesema endapo wakipewa ruhusu kutoka kwa UN watafanya hivyo
lakini kwa sasa hawawezi kutokana na sheria zilizopo.
Aidha kanali
mgawe ameongeza na kusema miili ya wanajeshi hao saba hivi sasa inafanyiwa
uchunguzi na timu ya wataalamu ya umoja wa mataifa na kisha baada ya hapo
italetwa nchini ambapo itahifadhiwa katika hospitali ya lugalo na kisha baadae
kupelekwa wizara ya ulinzi kwa ajili ya heshima za mwisho kwa ndugu, jamaa na
marafiki.
Ili kubaini chanzo
cha kuuwawa kwa askari hao, tayari jeshi la wananchi limeteua timu ya wataalamu
ambayo itaelekea Darfur kuchunguza kwa kina mauaji hayo ambayo ni makubwa
kutokea kwa askari wanaolinda amani wa umoja wa mataifa.
Umoja wa Mataifa waaswa
Umoja wa
mataifa umetakiwa kuangalia usalama wa wanajeshi wanaolinda amani katika sehemu
mbalimbali duniani ili kuzuia wanajeshi hao kuendelea kushambuliwa na hatimaye
kuuwawa pindi wanapokuwa kazini.
Kauli hiyo
imetolewa na mhadhiri mwandamizi wa sayansi ya siasa na utawala kutoka chuo
kikuu cha Dar es Salaam, Dr Lupa Ramadhani wakati akielezea tukio la kuuwawa
wanajeshi saba watanzania mjini Darfur nchini Sudan.
Dr Lupa
ameutaka umoja wa mataifa kutunga sheria zitakazozidi kuwalinda wanajeshi
wanaolinda amani ikiwezekana kulegeza sheria za sasa zinazowazuia wanajeshi
kupambana na waasi.
Kuhusianan
na mahusiano ya kidiplomasia kati ya tanzaia na sudan kusini, Dr Lupa amesema
shambulizi hilo haliwezi kuathiri urafiki uliopo baina ya nchi hizo kwani hata
waasi hao hawatambuliwi na serikali ya sudan kusini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment