Ramani ya Uganda
Moto mkubwa uliowaka baada ya ajali mbaya ya barabarani iliohusisha lori la mafuta, umewaua takriban watu 33 mjini kampala Uganda ambapo Watu wengine 30 wanadaiwa kujeruhiwa vibaya kufuatia tukio hilo.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa kati ya waliofariki ni raia waliokuwa wakikimbilia eneo hilo la tukio kwa lengo la kutaka kuteka mafuta yaliokuwa yakivuja kutoka kwenye lori la mafuta lililopata ajali.

Maafisa wa serikali walikuwa katika harakati za kutambua mili ya waliofariki ingawa miili ya wengi wao ilikuwa imechomeka vibaya.

Idara ya polisi imesema kuwa waliofariki waliteketea kiasi cha kutotambulika na itabidi watumie utaalamu wa vinasaba au DNA kutambua miili ya waliokufa.
Chanzo: BBC: Swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top