Maafisa wa Afya Misri wamesema takriban watu 42
wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo
wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua
wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300
wamejeruhiwa.
Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa
Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia.
Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.
Katika kikao na waandishi wa habari,
wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Sisi na
kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia wenzake.
Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.
Waandamanaji hao wanasema vikosi maalum
viliwafyatua risasi baada ya swala ya fajir huku wengine wakishambuliwa
walipokusanyika nje ya makao ambako bwana Morsi anadhaniwa kuzuiliwa
wakitaka watawala kumwachilia huru.
Msemaji wa chama cha Muslim brotherhood amesema
kuwa idadi ya waliofariki katika ghasia hizo imefikia 30 huku zaidi ya
watu 500 wakijeruhiwa.
Lakini katika taarifa yake, jeshi la nchi hiyo
limesema kuwa kundi moja la kigaidi lilikuwa likijaribu kuingia katika
kambi hiyo na kumuua mwanajeshi mmoja.
Limeongezea zaidi ya watu 200 walitiwa mbaroni wakimiliki silaha kama vile visu.
Duru kutoka wizara ya afya zilisema kuwa afisaa mmoja wa jeshi aliuawa.
Bwana Morsi, aliyekuwa rais wa kwanza wa
kiisilamu kuchaguliwa kidemopkrasia Misri, aling'olewa mamlakani na
jeshi, siku ya Jumatano baada ya kufanyika maandamano makubwa.
Mmoja wa waandamanaji Mahmud al-Shilli, aliambia
shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi waliwarushia gesi ya kutoa
machozi lakini kikundi cha wanaume waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia
ndio waliwafyatulia risasi.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye vyombo vya
yhabari vya serikali, jeshi lililaumu kikundi cha watu wlaiokuwa
wamejihami ambao limesma ni mgaidi waliokuwa na njama ya kuvamia kambi
ya jeshi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment