Mkuu wa jeshi nchini Misri, Abdel Fattah al-Sisi akihutubia muda mfupi kabla ya jeshi kupindua nchi July 3, 2013 
Mkuu wa jeshi nchini Misri, Abdel Fattah al-Sisi akihutubia muda mfupi kabla ya jeshi kupindua nchi July 3, 2013.
 
Umoja wa Afrika umesimamisha kwa muda uanachama wa  Misri katika umoja wake jana (Ijumaa) baada ya kutimuliwa madarakani kwa Rais Mohamed Morsi, kulingana na sheria zake  kali dhidi ya mabadiliko ya serikali kinyume cha katiba.

Afisa wa AU amesema Baraza la amani na usalama la umoja huo liliamua kusimamisha ushiriki  wa Misri katika shughuli za umoja huo mpaka pale utaratibu wa kikatiba utakaporejeshwa.

Baraza la umoja wa Afrika lilikutana jana katika makao makuu ya AU nchini Ethiopia kujadili mzozo wa kisiasa wa Misri kufuatia kuondolewa kwa Morsi na jeshi siku ya jumatano.

Kutimuliwa kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia hakuendani na vipengele vya katiba ya Misri na badala yake inaangukia katika mabadiliko ya serikali kinyume cha katiba.

Kabla ya mkutano huo kamishna wa AU Nkosazana Dlamini Zuma alisisitiza msingi wa msimamo wa taasisi hiyo kwa mabadiliko kama hayo kwa serikali.

Hata hivyo balozi wa Misri katika umoja wa afrika Mohamed Edress alisema kabla ya maamuzi hayo kwamba sauti za mamilioni ya raia wa Misri lazima zisikike , zieleweke na kuheshimiwa. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top