Pumnzikeni kwa amani wapenzi!
Wapenzi wawili huko Congo waliamua kuchukua jukumu la
kujinyonga kwa kujininginiza kwenye mti hadi kufa baada ya wazazi wa
mvulana kumkataza mtoto wao kumuoa msichana anayempenda.
Baada ya jitihada zao
za kuwashawishi wazazi kushindikana vijana hawa waliamua kuchukua hatua ya
kujinyonga....
Hii inaelekeana kwa kiasi fulani na kisa cha wale wapenzi wawili waliozikwa pamoja kwenye kaburi moja katika makumbusho ya Kaole Bagamoyo ambapo kaburi lao linaitwa kaburi la wapendanao.
Ni kaburi linalovutia watu wengi wa ndani na nje ya nchi kutokana na aina ya kifo chao kilivyotokea ambapo walikutwa wamekufa baharini wakiwa wamejifunga pamoja.
Hakika walipendana ndio mana siku ya wapendanao kaburi hili huvutia watu wengi.
Kwa wenzetu huko Congo mambo ni tofauti kidogo hawakukumbwa na dhoruba ya baharini bali pingamizi la wazazi ambao hawakutaka vijana wao waoane hadi wakaamua kufa pamoja kwa kujinyonga. Walipendana.
Hii ni aina nyingine ya wapenzi na mapenzi inayoibua changamoto ya aina yake kwa wazazi na jamii. Hili ni somo jipya kwa familia.
NI TUKIO LA KUSIKITISHA.
NI TUKIO LA KUSIKITISHA.
chanzo:http://masainyotambofu.blogspot.com
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment