Kamati
ya Bunge la Uingereza limepokea taarifa kuwa zaidi ya dola milioni 650
pesa za msaada zilizotolewa na mataifa ya Ulaya kwa bara la Afrika
zimetumiwa vibaya.
Kamati ya bunge la malodi kuhusu maswala ya nje,
inachunguza jinsi ambavyo dola bilioni 1.3 zilizotolewa kama msaada kwa
miradi ya maji kusini mwa Jangwa la Sahara miaka kumi iliyopita,
zilivyotumiwa.
Matatizo yalitokana na mipango duni na hata wakati wa kuitekeleza miradi mipango haikuwa sawa.
Mkaguzi mmoja wa matumizi ya pesa aliambia
kamati hiyo kuwa utafiti wake ulionyesha wazi hali ya miradi mingine
ambayo ilifanywa na Muungano wa Ulaya katika mwongo mmoja uliopita.
Miradi ya maji hujumuisha utoaji wa huduma za maji safi, ujenzi wa vyoo hatua ambazo zinazuia kulipuka kwa magonjwa.
Wakaguzi pia waligundua kuwa vifaa vilivyonunuliwa na mameneja wa miradi kama paipu vilikuwa vinahitajika.
Matatizo yanatokana na ikiwa miradi hiyo inaweza kudumu au la.
Katika visa vingine, idadi ya wenyeji wanaopokea mafunzo ni ndogo sana kwa hivyo baada ya miradi kutekelezwa haiwezi kudumu.
Lakini tatizo kubwa zaidi lilikuwa ufadhili au
kuwepo mikataba ya kudumu kutoka kwa kamati na serikali za nchi maskini
kuhusu namna ya kufadhili mfano hiyo miradi ya maji.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya ustawi Mark Doyle
anasema kuwa ikiwa mikataba haiwezi kuwekwa wazi basi itakuwa vigumu kwa
matumizi mazuri ya pesa na pia kuna hatari ya pesa za maendelo kuendelea
kufujwa.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment