Leo
asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la
kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa
kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka
wa serikali.
Baada ya
kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka
mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa
kisheria, na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria
wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya
matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko
huru na hana kesi ya kujibu..
My take:Polisi
na serikali, mnaendelea kujidhalilisha kwa kufungua kesi ambazo
zinaendelea kuwavunjia heshima, acheni kufuata maelekezo ya kina
Mwigulu, hawajui sheria, hawajui misingi ya kufungua kesi, nyie kila
siku mtakuwa mnafungua kesi mpaka lini wakati mnashindwa daima mbele ya
mahakama na umma wa wa-Tanzania.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment