Mkutano wa majadiliano ya kimataifa kuhusu matumizi ya teknolojia katika kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika umeanza rasmi jijini Dar es Salaam ukiwashirikisha zaidi ya washiriki 800 wakiwemo marais tisa na viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali.
Mkurugenzi mkuu wa tume ya taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH Dakta Hassan Mshinda amesema Lengo la mkutano huo wa majadiliano ni kubadilishana mawazo kutathmini namna ya kutumia teknolojia na kufanikiwa katika mambo kadhaa ikiwemo nishati, afya, elimu, kilimo, bandari, reli na barabara.
Tayari tume ya taifa ya sayansi na teknolojia imekwishatoa mafunzo kwa wataalam wa Tanzania wanaotoka sekta mbalimbali wanaoshiriki kwenye majadiliano hayo ili kubadilishana mawazo na wataalam wengine kutoka nje ya nchi.

Miongoni mwa marais wanaoshiriki mkutano huo utakaodumu kwa siku tatu jijini Dar es Salaam ni pamoja na marais wa Kenya, Uganda, Benin, Gabon, Comoro, Burkinafaso pamoja na Togo na marais wastaafu, mawaziri wakuu, mawaziri pamoja na manaibu waziri.
0 comments:
Post a Comment