Wanajeshi wa Nigeria
Serikali
ya Nigeria imetuma kikosi kikubwa cha wanajeshi pamoja na silaha kukabiliana na
wapiganaji katika majimbo matatu ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa
kutoka kwa serikali ilisema kuwa nia ya kutumwa kwa wanajeshi hao ni kuweza
kupata tena udhibiti wa sehemu ambazo inaaminika ziko chini ya udhibiti wa
wapiganaji hao, pamoja na kuimarisha usalama.
Mnamo
Jumanne Rais Goodluck Jonathan, alitangaza hali ya hatari, katika majimbo
matatu ya Yobe, Borno na Adamawa baada ya majimbo hayo kushuhudia mashambulizi
mabaya sana.
Wapiganaji
kutoka kundi la Boko Haram, wanalaumiwa kwa kufanya mashambulizi hayo.
Kundi
hilo ambalo lina mizizi yake Kaskazini mwa Nigeria,limehusishwa na mauaji ya
watu 2,000 tangu mwaka 2010.
Boko
Haram, limedhibiti baadhi ya sehemu za kaskazini mwa nchi, kwa miaka mitatu
iliyopita na nyingi ya ghasia wanazofanya zimekuwa sana sana katika eneo hilo.
Hakuna
shaka kuwa hali Kaskazini mwa Nigeria inaendelea kuzorota na sasa rais Goodluck
Jonathan amekiri hilo. Hakuna yeyote serikali angeweza kulitamka hilo.
Ukubwa
wa mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram, umelazimisha rais Jonathan kuchukua
hatua na hata kuwanyamazisha baadhi ya wakosoaji wake wanaosema kuwa
amejikokota kuchukua hatua.
Baadhi
ya wadadisi wamependekeza kuwa ikiwa hali itaandelea kuzorota hivyo, itakuwa
vigumu kukabiliana na kundi la Boko Haram na litaweza hata kuunda taasisi zake.
Je,
wanajeshi zaidi wataweza kukabiliana na hali? kikubwa ni ambavyo wanajeshi hao
wataendesha harakati zao.
Wadadisi
wanasema kuwa , jeshi lina kibarua kigumu kwani kuna dalili tayari limeshindwa
katika vita hivi, na raia wanahisi kuwa katikati ya mtego Nigeria
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment