TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Justine Peter Mwandu kuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Taarifa
iliyotolewa leo, Ijumaa, 03 Mei, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Aprili 28,
mwaka huu, 2013.
Kabla
ya uteuzi huu, Ndugu Justine Peter
Mwandu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika Shirika hilo.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
03 Mei, 2013
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment