Asasi ya Vijana wa umoja wa Mataifa Tanzania [ YUNA] imejipanga kukusanya maoni kwa vijana nchini ili kuhakikisha wanapata mawazo ya vijana hao ambayo watayawakilisha katika Umoja wa Mataifa katika kufikia malengo ya Mellenium.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bwana LWIDIKO EDWARD ameelezea jitihada ambazo wamekuwa wakizichukua katika kuhakiki vijana wanahusishwa zaidi katika kufikia malengo ya Milenium ikiwemo kuzunguka zaidi ya mikoa sita nchi nzima kwa kuwahusisha wanafunzi wa vyuo na Sekondari.
Mwenyekiti wa Umoja huo ameendelea kufafanua kuwa pamoja na Mlengo ya Melinia kuwa na mipango na malengo mengi lakini bado vijana wameonekana kuachwa katika malengo hayo hivyo ili kuhakikisha vijana wanaingizwa katika malengo ya melinia yajayo wameandaa mkutano Mjini DODOMA Katika Jengo la Bunge.
Kwa upande wa atakatayekuwa kiongozi wa Mkutano huo CATHERINI FIDELIS, amesema kuwa nikkwumalayakwanza vijana wa Tanzania kupata Fursa ya kuanda mukutano huo utakaofanyika Tarehe 2 mpaka tarehe 6 ya mwezi ujao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment