Chama cha wanasheria wanawake hapa nchini TAWLA , kimewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika mabaraza ya katiba ili waweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuandaa katiba mpya.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama cha wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade katika mkutano ulioandaliwa na chama hicho na kuwashiriksha madiwani na wanaharakati wengine juu ya ushirikishwaji wa wanawake katika katiba mpya.
 
Akiongea na waandishi wa habari pembeni  mwa mkutano huo, Bi Aisha Bade amesema endapo  wanawake watajitokeza na kujiandikisha ili kugombea nafasi za kuwamo katika mabaraza ya katiba ya maeneo wanakoishi itawasaidia sana katika kutetea maslahi yao na mambo yanayowapa changamoto kama umiliki wa ardhi.

Naye Magdalena Rwebangira ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa asasi za jinsia katika katiba amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wanawake ni kujitambua na kujiweka nyuma katika mambo yanayowagusa moja kwa moja.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa blue pearl ubungo plaza ulikuwa na nia ya kutoa elimu ya katiba kwa wanaharakati na madiwani ambao watajumuishwa katika mchakatowa kupata mabaraza ya madiwani. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top