Rais wa CWT Mwalimu Gratian Mukoba
Baraza la Taifa la chama cha walimu Tanzania(CWT) limeishauri serikali kuwalipa walimu madai yao mbalimbali ili kuepuka mgogoro mwingine baina ya pande mbili hizo.Hayo yamesemwa na Rais wa CWT Mwalimu Gratian Mukoba kuwa serikali inadaiwa zaidi ya sh 25 bilioni zinazotokana na kutolipwa kwa malimbikizo ya mishahara na madai mengine kama likizo, uhamisho,gharama za masomo pamoja na matibabu .
Aidha mukoba amesema kuwa zaidi ya walimu 60,000 wanaostahili kupandishwa madaraja hawajapandishwa wakati bunge lilipitisha fedha za kupandisha walimu kuanzia julai 2012 na kusema kuwa baraza lilipokea kwa masikitiko ahadi iliyotolewa na wizara ya elimu na mafunzo ya kutatua kero hiyo kwa walimu. Amesema kuwa kero hizo zilitakiwa kutatuliwa desemba 2012 lakini kutokana na wizara kushindwa kutekeleza ahadi hiyo baraza la Taifa CWT limeazimia kuwa mkuu wa utumishi wa umma kumfuatilia katibu mkuu wa wizara ya elimu kutekeleza ahadi hiyo ifikapo machi 2013.
Pamoja na hayo mukoba amesema kuwa chama kinatambua kwa rufaa ya kupinga hukumu ya jaji wambura wa mahakama kuu Divisheni ya kazi ya kuzuia mgomo wa walimu na kusema kuwa chama kinazingatia agizo la mahakama la kutaka pande zote kurudi mezani kwa majadiliano.
Baraza la Taifa la chama cha walimu Tanzania(CWT ) liliazimia hayo kwenye kikao kilichofanyika tarehe 16-20 januari mjini Dodoma. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment