Dawa ya Tamiflu
Wanasayansi nchini Uingereza wamesema serikali
duniani zinapoteza mabilioni ya fedha kwa kuhifadhi dawa za tibu homa ya
mafua makali, dawa ambayo matokeo yake yanatiliwa mashaka.
Serikali mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza
zilihifadhi dawa ya Tamiflu katika bohari zao, huku kukiwa na wasiwasi
wa kutokea mlipuko wa mafua ya ndege.
Watafiti kutoka kampuni ya dawa ya
Cochrane Collaboration na jarida la masuala ya utabibu la British
Medical Journal, wamesema hakuna ushahidi mzuri unaobainisha kuwa dawa
ya Tamiflu imepunguza idadi ya watu wanaougua na kulazwa hospitali au
madhara yanayosabishwa na virusi vya mafua.
Wamesema kama kuna faida ya dawa hizo basi ni ndogo lakini kuongeza hatari ya mafua.
Hata hivyo kampuni inayozalisha dawa hizo, Roche
na watalaam wengine wamesema uchambuzi huo una dosari, huku wakisema
kimsingi haikubaliani na utafiti huo.
Uingereza imetumia pauni £473m kununulia dawa ya
Tamiflu, ambayo imejazana katika bohari za dawa duniani kote kujiandaa
kwa mlipuko wa mafua makali.
Dawa hiyo ya Tamiflu imekuwa ikihifadhiwa nchini
Uingereza tangu mwaka 2006 wakati baadhi ya mashirika yalikuwa
yakitabiri kuwa ugonjwa wa mafua ya ndege ungeweza kuua watu wapatao
750,000 nchini Uingereza. Uamuzi kama huo ulifanyika katika nchi
nyingine duniani.
Dawa hiyo ilishauriwa kwa kiasi kikubwa itumike wakati wa mlipuko wa mafua ya nguruwe mwaka 2009.
Kampuni za dawa hazichapishi taarifa zao zote za
utafiti. Ripoti hii ni matokeo ya mvutano kuhusu taarifa iliyofichwa
zamani kuhusu ufanisi na madhara ya dawa aina ya Tamiflu.
Ripoti hiyo imehitimisha kuwa dawa hiyo
ilipunguza dalili za homa ya mafua kutoka siku saba hadi siku 6.3 kwa
wakubwa na kwa watoto siku 5.8.Taarifa ya wahariri wa ripoti hiyo
wanasema dawa kama paracetamol zingeweza kuwa na ufanisi sawa na hiyo.
Kuhusu madai kwamba dawa hiyo ilizuia madhara ya
pneumonia, Cochrane wanasema majaribio hayo yalikuwa dhaifu sana kiasi
kwamba "hakuna matokeo mazuri yaliyobainika".
Carl Heneghan, Profesa wa Evidence-Based
Medicine katika chuo kikuu cha Oxford na mmoja wa wahariri wa ripoti
hiyo ameiambia BBC: "Nafikiri fedha yote £500m haijanufaisha afya ya
binadamu na huenda tumewadhuru watu kutokana matumizi ya dawa hizi.
Chanzo: BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment