Rais Jakaya kikwete anaendelea kulihutubia Bunge Maalumu la katiba ambapo amesema:

Akili za kuambiwa changanya na zako. Usisubiri kuambiwa tumia akili yako.

Tengenezeni katiba ambayo haitahitaji kufanyiwa mabadiliko katika kipindi kifupi kijacho, jukumu hili mnalo. Hakikisheni kuwa mnaitumia vyema fursa hii. Jiridhisheni kuhusu uandishi. Inasemekana Rasimu hii ina utitiri wa mambo ambapo mengine yalipaswa kuwa katika sera kwa utekelezaji.

Baadhi ya vifungu vina mapungufu yake. mfano, Rasimu imetambua sehemu za maji za bahari lakini ilisahau sehemu za maji zinazotenganisha Tanzania na jirani zatu mfano Maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Mgongano kuhusu muundo wa muungano. Kuna mambo ya serikali washirika kuingizwa katika muungano. mfano, kilimo, ufugaji, uvuvi, elimu, pembejeo na yafananayo na hayo. Hivto ikiwa mnahitaji mmundo wa serikali tatu hamna budi kuyaondoa. Lakini kama mnataka muundo wa serikali mbili mambo haya yanatekelezeka bila tabu.

Katika suala la muungano wamesahau suala la muhimu la utumishi mfano majeshi.

Yatazameni mambo haya kwa makini mnaweza kuyagundua na mengineyo.

Fanyeni uchunguzi wa kutosha kuhusu dhana mpya ambazo hazikuwepo awali. Mfano: Ibara 128 (iid). inayohusu nafasi ya ubunge.

Ukomo wa vipindi vitatu kwa mbunge. Rasimu haisemi vitatu mfululizo. Jiridhisheni juu ya ukomo huu. "Kwa uzoefu wa dunia ukomo unawekewa wakuu wa nchi". Duniani hawaweki ukomo kwa wabunge, Tanzania tunataka kuwa wa kwanza.

Si suala la kujadili serikali mbili au tatu tuu bado kuna mambo mengi yanahitaji kuangaliwa kwa makini.

Utaratibu wa kumuondoa mbunge katikati ya kipindi chake. Tafakarini vyema athari zake. Dhana ya mbunge anapopoteza ubunge chama chake kujaza nafasi linahitaji kuangaliwa kwa makini pia.

Muundo wa serikali tatu badala ya mbili za sasa umevuta hisia za watu wengi. Umekuwa mkali kwa kila pande zote. Msidhani avumaye baharini ni papa tuu, wapo wengine pia. Ombi langu, kuweni watulivu mnapolijadili jambo hili. mkilijadili kwa jazba wenye hasira hawajengi. Epukeni jazba ili mfanye uamzi ulio sahihi kwani kinyume chake ni matatizo makubwa kwa nchi.

Kama alivyosema Jaji Warioba, suala la muundo wa serikali tatu sio mara ya kwanza kuzungumzwa. Ni jambo linalokwenda na kurudi. Inafurahisha mnapolijadili, mlijadili na kufikia muafaka ili tuanze na mambo mengine.

Wapeni heshima waasisi wa muungano.

Tume imetoa hoja kuu mbili kuhusu muungano. Kwanza ni idadi kubwa ya watanzania kuunga mkono muundo wa serikali tatu. Pili muundo wa serikali tatu unatoa suluhisho la matatizo mbalimbali kuhusu kero za muungano. Kuna wanaunga mkono muundo huu.

Wanaoupinga muundo wa serikali tatu wanadai kuwa takwimu hazioneshi ukweli wenyewe. Kama muundo wa muungano ni kero kwa watanzania ingethibitika kwa idadi ya walioujadili.

Zipitieni kwa makini changamoto hizi na kuona ni muundo upi unafaa. Uamuzi ni wenu. Katika kujadili changamoto hizi mtafute majawabu ya changamoto hizi, sio ndogo.

Wanaotetea mfumo wa serikali mbili wanaona kuwa mfumo wa serikali mbili unafaa, una gharama zake hivyo mfumo wa serikali tatu itakuwa zaidi. Vilevile kero za muungano zinaweza kuondolewa. Changamoto zilikuwa 31 kwa sasa zimebaki sita.

Mimi ninaishi kwa matumaini lazima tujipe matumaini kwamba kuna tunayoweza kuyafanya. Mimi naamini na wapo wanaoamini.

22 badala ya 11 ya awali. Kinachowezekana kipunguzwe. Kuongezwa kwa kipengele chochote hakukuwa kwa hila bali kulifanyika kwa uwazi pasipo kificho. Kulishirikisha pande zote mbili na wabunge waliridhia.

Mambo ya uchumi sio ya muungano. 
CCM inaamini inaweza kuondoa kero za muungano pasipo kuhitaji serikali ya tatu. Haya ni maneno yangu. Bunge hili ni kazi yake.

Serikali ya muungano haina dhamana hivyo haikopesheki labda idhaminiwe na serikali mojawapo kati ya serikali washirika mfano Tanganyika ambayo ina vyanzo mbalimbali vya mapato. Yawekeni sawa haya.

Mkiamua serikali tatu chagueni mfumo utakaoufanya ajisimamie.

Tutaendelea kukujuza.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top