Wanamgambo wa kiislam nchini Somalia wameshambulia
hoteli moja muhimu katika eneo la Kati mwa Somalia ambalo wanamgambo hao
walipoteza udhibiti wake wiki iliyopita.
Walioshuhudia shambulio hilo wameiambia BBC kuwa
gari lililipuka nje ya hoteli hiyo katika mji wa Bulo-burde wanakoishi
askari wa muungano wa Afrika na makamanda katika jeshi la Somalia .
Mlipuko huo ulifuatiwa na makabiliano ya risasi yaliyodumu kwa muda wa saa tano .
Walioshuhudia wanasema takriban watu kumi na
wanne wameuawa katika shambulio hilo , ambalo wapiganaji wa al-Shabab
wamesema walilitekeleza.
Mji wa Bulo-burde ulitwaliwa tena katika moja ya
harakati za kijeshi zinazoendeshwa na vikosi vya Amison na vile vya
serikali dhidi ya wanamgambo hao.
Chanzo: BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment