Dk. Ferdinand Massau.
Daktari huyu amenyanyasika kwa sababu ya uzalendo na huruma yake kwa
Watanzania masikini, hadi yamemfika na amepoteza uhai wake. Pengine kwa
‘kupigwa kwake sisi tutapona’.
Dk. Masau alikuwa mmoja wa wataalamu wachache wa upasuaji wa moyo,
kujitoa kufanya kazi ya kuhudumia wagonjwa wa moyo hapa nchini, tena
masikini bila malipo, akijitahidi kwa kushirikiana na marafiki zake
kutoka Ujerumani, Marekani na Uingereza kutoa huduma za matibabu ndani
ya nchi yetu badala ya kuingia gharama kubwa kwenda nchini India.
Baadhi ya viongozi wa serikali na wahudumu wa Wizara ya Afya hawakufurahishwa na mpango wa kuhudumia wagonjwa hapa nchini na kuokoa mabilioni ya fedha zilizokuwa zikipelekwa nchini India kwa sababu gawio la asilimia 10 halitapatikana tena.

Kwanini nasema ni baadhi ya watu walioko serikalini? Ni kwa sababu
serikali haikutaka kujihusisha au kujali mgogoro uliokuwa ukiendelea
kati ya THI na NSSF, hata siku ambayo wagonjwa walitakiwa kutolewa nje
pale THI serikali ilikaa kimya.
Hatutakiwi kulalamikia uamuzi wa mahakama, lakini inapotokea utu
umekosekana dhamira zinatuuma. Asiyeumwa na dhamira ana tatizo kiroho
au kinafsi.
Tujiulize ni Watanzania wangapi masikini ambao wakienda Wizara ya Afya
kuomba msaada wa kupelekwa India kwa matibabu wanapata? Je, ni
wafanyakazi wangapi wa serikali wa kada za chini au kati ambao wakiugua
wanapelekwa India? Lakini kama kuna matibabu ya bei nafuu hapa Tanzania
ambayo serikali imetoa msamaha wa kodi kwa vifaa vyake au inatoa
ruzuku wananchi wanaweza kutibiwa na kuokoa maisha yao.
Kifo cha Dk. Masau si kwamba kimetushtua Watanzania tu bali hata
wageni. Ni mtu aliyeona mbali, aliyefikiri juu ya kulisaidia taifa lake
na kurudisha fedha ndani kwa ajili ya kukuza uchumi na ustawi wa afya za
jamii. Lakini wale waliopewa dhamana wameamua kummaliza ili wafaidi
asilimia 10. Hii ni laana na damu za wagonjwa waliokuwa wakipata
matibabu katika Taasisi ya Moyo nchini itawalilia wao na kizazi chao.
Kwanini tunakosa utu, huruma? Tunafikiri kuwa fedha za duniani zitatufikisha mahali? Watu wangapi wameondoka duniani wameacha matrilioni ya fedha? Yuko wapi bilionea aliyekuwa Rais wa Libya Hayati, Muammar Gaddafi? Wako wapi matajiri wa Kitanzania masikini walioishi kama miungu watu hapa duniani? Si kwamba hata magari au ndege zao zinawageuka na kuwaua? Tumuogope Mungu mwenye nguvu.

Malengo ya Dk. Masau katika taasisi ya THI yalikuwa kuwafanyia
uchunguzi na upasuaji wa moyo walengwa, hasa watu masikini wa
Tanzania. Kama alivyoandika kwenye tovuti ya THI; “Overall diagnosis as
well as surgery of heart related disease are our targets, especially to
poor people.”
Inasikitisha kuwa lengo hili lilipigwa vita na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakakubali kutumika vibaya kumfukuza katika taasisi hiyo huku wakilazimisha wagonjwa waliokuwa wamelazwa na dripu zao kutolewa nje.

Mara kadhaa kesi zimeendelea mahakamani, huku Dk. Masau akiwa
ameshalazwa rumande kwa kesi yenye mahusiano na THI, lakini mwishowe
Julai 10, 2012 taasisi ilifungwa rasmi na mali zake zote kupigwa mnada
na Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi.
Tunajiuliza wanaopiga mnada mali za kuhudumia wagonjwa wanawatumikia Watanzania gani? Je, wanastahili kuendelea kuitwa Watanzania? Je, kama Shirika la Hifadhi ya Jamii ambalo Watanzania wameweka fedha zao linashindwa kutafakari umuhimu wa ustawi wa afya za watu wake linawatumikia kina nani? Si kwamba fedha hizo ni bora zingechelewa kutoka THI kuliko kuwekeza kwenye majengo ya watu binafsi na wafanyabiashara? Ona sasa kazi waliyoianzisha ya kukwamisha utaalamu wa Dk. Masau imekamilika.

Huyu Dk. Masau ni Mtanzania masikini aliyethubutu kujaribu kitu kipya
kwa ajili ya Watanzania wenzake, akapigwa vita hadi kupoteza uhai wake
kwa msongo wa mawazo. Je, wataalamu wengine wazawa watakubali kurudi
nchini? Si kwamba kila mtu akikumbuka yaliyomkuta Dk. huyu atabaki huko?
Sote tunajua kuwa matibabu ni gharama, hususani ya upasuaji wa moyo,
misuli na mifupa. Lakini gharama za safari na kuishi nchi jirani,
kutafuta hati ya kusafiria na visa zinamuongezea mgonjwa mzigo mkubwa.
Kwa sasa ukitaka kupata matibabu ya bei nafuu kabisa nchini India si chini ya dola za kimarekani 10,000 sawa na sh mil. 16.3, pamoja na kulala na kula kwa siku 14 utakazokaa hospitalini. Je, Watanzania wangapi wanamudu gharama hizi?

Kosa kubwa la Dk. Masau ni kuthubutu kwa mafanikio kiasi kutibu
ugonjwa wa moyo kwa upasuaji nchini, lakini tutamkumbuka na bila shaka,
ipo siku tutajenga THI nyingine na itaitwa kwa jina lake. Buriani Dk.
Masau Watanzania masikini watakukumbuka daima.
Lakini ufisadi wa aina hii nao utafikia mwisho pale Mwenyezi Mungu atakapoamua na kusema HAPANA!
Via Tanzania Daima Jumapili
Via Tanzania Daima Jumapili
0 comments:
Post a Comment