Rais Joseph Kabila 
Maelfu ya watu wameandamana nchini Jamhuri ya kidemorasi ya Congo wakimpinga rais wa taifa hilo Joseph Kabila.

Wafuasi wa upinzani wanataka rais Kabila kuondoka madarakani wakati muhula wake wa pili wa uongozi utakapokamilika mnamo mwaka 2016.

Kuna shaka kuwa huenda katiba ikabadilishwa ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu.

Maandamano kwenye mji mkuu Kinshasa yaliripotiwa kuwa ya amani lakini polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kwenye mji wa Goma ulio mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Joseph Kabila alichukua mamlaka mwaka 2001 kufuatia kuuawa kwa babake Laurent Kabila.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top