Nchi 10 za kiarabu zimekubaliana kuisaidia Marekani kupambana na Islamic State.

Taarifa hii inafuatia mkutano wa viongozi wa nchi hizo ikiwemo Saudi Arabia na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry mjini Jeddah.

Nchi hizo pia zimekubaliana kusimamisha misaada ya kifedha na nguvu kazi ya wapiganaji kwa kundi la Islamic State ambalo linashikilia maeneo makubwa katika nchi za Syria na Iraq.

Hata hivyo Bwana Kerry ametoa changamoto kwa nchi hizo za kiarabu kuwa zinapaswa kusaini makubaliano ya muungano wa kimataifa dhidi Islamic State kwa sababu wamekwisha tambua hatari mbele yao.

Mkutano baina ya Waziri huyo na viongozi wa eneo hilo la mashariki ya kati umekuja siku moja tu baada ya tangazo la Rais Barack Obama la mpango wa kujenga mshikamano dhidi ya kundi la Islamic State kwenye nchi za Syria na Iraq.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top