Polisi nchi Marekani wametoa taarifa za kumhusu mwanzilishi wa kituo cha maonyesho na mtunza Tembo kutoka nchini Marekani ambaye pia ni mmiliki wa nyumba ya matumaini kwa Tembo, amefariki dunia baada ya Tembo aliyekua akimhifadhi kumkanyaga kwa bahati mbaya.

Vetenari James Laurita, aliyekuwa na umri wa miaka 56, alianguka alipokua katika kituo hicho cha matumaini kwa Tembo waliotelekezwa na kupoteza maisha yake alipokanyagwa na Tembo mmoja. 

Mapema wiki hii Laurita alikutwa akiwa hajiwezi katika kituo hicho yapata maili 87 sawa na kilomita 140 Kaskazini Mashariki ya Porland.

Inaelezwa kua alianguka kwa kichwa chake katika zege la kituo hicho na baada ya kunaswa, Tembo akamkanyaga kifuani kwa bahati mbaya.

''Tembo aliyemkanyaga hakuwa na hasira ,ilikua ni ajali kama ajali zingine,'' anaeleza bwana Mark Belserene wa kituo cha uchunguzi wa afya.

Inaelezwa kua baada ya uchunguzi wa kitabibu iligundulika kuwa sababu ya kifo cha Laurita ni kuvunjika mifupa kifuani pake na kukosa hewa ya kutosha.

Kituo hicho cha matumaini kwa Tembo na maonyesho na michezo mbali mbali ambacho si cha kujipatia fedha kilianzishwa mnamo mwaka 2011, ambacho kilipokea Tembo wake wa kwanza waitwao Opal na Rosie mwaka uliofuata.

Mwanzilishi huyo Laurita alikua ni mpenzi wa wanyama wa aina zozote za wanyama, lakini kwa Tembo ndo mnyama aliyezidia kwa mapenzi yake.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top