Katika tukio la kwanza la aina yake mwanamziki mmoja nchini Ufarasa amefanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kooni huku akiimba.
Madaktari wanasema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuepuka kuharibu mishipa inayosaidia binadamu kutoa sauti.
Mwimbaji huyo Alama Kante, ambaye ni
raia wa Guinea anayeishi Ufaransa alipewa dawa za kumfanya asihisi
uchungu wakati upasuaji huo ukiendelea.
Kante alikua na hofu kuhusu kupoteza sauti yake
kutokana na upasuaji huo lakini daktari wake akapendekeza aimbe huku
akipasuliwa ikiwa ni mara ya kwanza hatua kama hiyo kuwahi kuchukuliwa
kote duniani.
Profesa Giles Dhonneur, aliyeongoza upasuaji huo
katika hospitali ya Henri Mondor hospital, ameonyesha video ya
mwanamziki huyo akiimba huku naye akiendelea na upasuaji. Ameelezea
matuamani kuwa mambo yatakuwa sawa.
Amesema ni uchungu sana kufanya upasuaji kama
huo bila kutumia dawa ya kumfanya mgonjwa asihisi uchungu lakini mbinu
na dawa aliyotumia ilimuwezesha Kante kuhimili bila matatizo yoyote.
Kante ambaye amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na alipoamka na kuzungumza tena madkatari na wauguzi walifurahi sana kutimiza lengo lao.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment