Mchungaji Langeni Mwasibira wa Baptist Church lililopo Kyela mkoani Mbeya amelazimika kuondoka hospitalini Muhimbili jijini Dar es Salaam kurejea nyumbani baada ya kuambiwa ugonjwa wake…

Mchungaji Langeni Mwasibira (39) wa Baptist Church lililopo Kyela mkoani Mbeya amelazimika kuondoka hospitalini Muhimbili jijini Dar es Salaam kurejea nyumbani kusubiri kufa baada ya madaktari kumweleza wazi kuwa ugonjwa wake hauwezi kutibika.
 
Mchungaji Langeni Mwasibira wa Baptist Church lililopo Kyela mkoani Mbeya amelazimika kuondoka hospitalini Muhimbili jijini Dar es Salaam kurejea nyumbani baada ya kuambiwa ugonjwa wake hautibiki.
Gazeti hili liliwahi kuandika habari za Mchungaji huyo katika toleo namba 842, wakati huo waumini wake walipoamua kufunga na kumfanyia maombi kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya.

Mchungaji huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kisyosyo kata ya Matema, Kyela anasumbuliwa na ugonjwa ujulikanao kwa jina la Nerofibroma, alisema anafanya utaratibu wa jinsi ya kuondoka kwenda kwao.
 
Mchungaji Langeni Mwasibira akiwa katika hospitalini ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
“Nimeteseka kwa muda mrefu sana bila kupata nafuu, gonjwa hili lilinianza mwaka 1994 kama doa jeusi, baadaye ukatokeza upele, nilipoenda hospitali yetu ya wilaya ya Kyela hawakugundua tatizo, ilibidi niende hospitali ya rufaa ya Mbeya mwaka 1998.

“Katika hospitali hiyo nayo walishindwa, hawakuniambia kinachonisumbua, uvimbe, muwasho na maumivu makali yaliongezeka, ilibidi walipasue lakini hakukuwa na nafuu, bali ndipo ulizidi kuumuka na maumivu yasiyo na kifani.”
Kwa walioguswa na habari hii wanaweza kuwasiliana au kumsaidia mchungaji kupitia namba zake ambazo ni 0758 902884 au 0786 557612
GPL  TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top