Polisi huko Ireland Kazkazini
wamemkamata mwanasiasa mashuhuri wa chama cha Sinn Fein ,Gerry Adams kwa
kuhusishwa na mauaji yaliyotokea yapata zaidi ya miaka 40 iliyopita.
Adams anahojiwa kuhusu mauaji ya Jean McConville
ambaye alitekwa nyara na kundi la waasi la IRA mnamo mwaka 1972 na kisha
akapatikana amepigwa risasi na kuuawa .
Kiongozi
huyo amekanusha kuhusika kivyovyote vile akisema kuwa alijipeleka
binafsi kuzungumza na polisi ili kujaribu kusuluhisha madai hayo
yaliyomwandama kwa miaka mingi mno .
Adams anakanusha kuhusika kwa vyovyote vile na utekaji nyara wala mauaji yake bi McConville ambaye alikuwa mama wa watoto kumi .
Adams anazuiliwa kutokana na kifo cha mjane huyo aliyetekwa nyara na kundi la IRA mwaka wa 1972 .
Madai haya yanafwatia mahojiano mjini Belfast
mwaka wa 2001-2006 baina ya chuo kikuu cha Boston Marekani na
wakereketwa wa vita hivyo vilivyonuiwa kuikomboa Ireland kutoka kwenye
minyororo ya ukoloni.
Mahojiano hayo yalifanywa kwa misingi kuwa
mahojiano hayo yangewekwa siri hadi baada ya vifo vya wahusika
wakuu, lakini baada ya kesi za kutaka kutambulika wahusika na waathiriwa
waliotoweka wakati wa vita hivyo chuo hicho kililazimishwa kutoa sehemu ya mahojiano kwa serikali ya Ireland.
Mmoja kati ya watu 16 waliosemekana kutoweka ni bi McConville .
Mjane huyo alilaumiwa na IRA kuwa mpelelezi wa
polisi lakini baada ya ufafanuzi wa polisi yapata mwaka wa 1999,
McConville ilibainika kuwa hakuwa.
Kundi hilo la IRA lilikiri kutekeleza mauaji
yake bi McConville mwaka wa 1999 lakini mwili wake ulipatikana mwaka wa
2003 ukiwa umetupwa kwenye ufukwe wa bahari.
IRA inashtumiwa kwa kampeini na mauaji yaliyotikisa Ireland kaskazini kwa takriban miaka thelathini.
BBC
0 comments:
Post a Comment