
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Raza azuru Australia
Waziri mkuu wa Malaysia Najib
Razak amewasili jijini Perth, magharibi mwa Australia, ambako shughuli
za kutafuta ndege ya MH370 inaendelea ilikuwashukuru wale wote
wanaohusika na shughuli yakusaka mabaki ya ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka majuma matatu yaliyopita .
Bwana Najib atakutana na waziri mkuu
wa Australia Tony Abbott na Angus Houstun ambaye ni mkuu wa mjeshi wa
aliyestaafu, wote wanasimaia shughuli hiyo.
Ndege hiyo ya Malayisa ilipotea tarehe nane
mwezi machi wakati ilipokuwa ikifanya safari ya kwenda Kuala Lumpur
kutoka mji wa Beijing. Ilikuwa imewabeba abiria 239.
Ndege na meli kadhaa zimekuwa zikizunguka eneo la kusini mwa bahari Hindi, ambako ndege hiyo inaaminika kuwa ilianguka.
Tayari meli moja ya Uingereza imewasili huko kuongeza nguvu katika juhudi hizo.

Jamaa wa ndege ya Malaysia MH370 waandamana
Mahala panapoendeshwa shughuli ya kutaifuta imepanuka hadi kilomita laki mbili magharibi mwa mji wa Perth nchini Australia.
Lakini kufikia sasa hakuna lolote lililoonekana kuasharia uwezekano wa ndege hiyo kupatikana pahala hapo.
Waziri mkuu Najib Razak wa Malysia amekukutana na kikosi kinachoendehsa shughuli hiyo asubuhi hii kabla ya kuendeleza kazi hiyo.
Pia waziri huyo atatembelea shirika linalo ongoza shughuli ya kutafuta ndege hiyo.
Familia na jamaa ya abiria 153 kutoka China
wameshtumu vikali serikali ya Malaysia kwa kutowapa habari zozote
kuhusiana na jamaa zao ambao walikuwa miongoni mwa abiria 239 waliokuwa
ndani ya ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Beijing Uchin.
BBC
0 comments:
Post a Comment