
Raia wa Kenya waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji
wa kiisilamu la Al Shabaab mwaka 2011 nchini Somalia, wameokolewa
na wanajeshi wa Kenya
Wakenya hao walikuwa wanafanyia kazi mashirika ya misaada ya kibinadamu .
Daniel Njuguna ambaye alikuwa
akifanya kazi katika shirika la Madaktari wasio na mipaka Medecins Sans
Frontieres MSF na James Kiarie wa Shirika la Care International,
walikaguliwa kiafya na walitarajiwa kupelekwa Nairobi.
Awali walikuwa chini ya uangalizi wa majeshi ya
Kenya ambao ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopo nchini
Somalia AMISOM.
Kenya ilipeleka majeshi yake kwenda nchini
Somalia mwaka 2011 kujiunga na AMISOM kufuatia matukio ya utekaji nyara
yaliyokuwa yakiendeshwa na wapiganaji wa Al shabaab katika mipaka ya
nchi hiyo na Somalia.
Majeshi ya AMISOM yakishirikiana majeshi yale ya
serikali ya Somalia yamekuwa yakiendesha mapambano dhidi ya wapiganaji
wa Al Shabaab ambao wanafadhiliwa na kundi la kigaidi la al Qaeda
linaloshikilia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment