Urusi imewakamata raiya 25 kutoka Ukraine
Kitengo cha kimataifa cha upelelezi Nchini Urusi FSB, kinasema kuwa kimewazuilia raia 25 wa Ukraine, kikiwalaumu kwa kupanga mashambulio ya kigaidi mwezi uliopita wakati jimbo la Crimea lililokoUkraine lilipokuwa likiandaa kura ya maoni.

Idara hiyo inasema watu hao wanaozuiliwa walikuwa wanachama wa vuguvugu la ultra-nationalist na walikuwa wakijiandaa kusababisha mashambulio hayo katikati na kusini mwa Urusi.
Kikosi cha polisi cha Berkut chalaumiwa kwa vifo wakati wa maandamano

Awali, waziri wa usalama wa taifa wa Ukraine, Arsen Avakov amesema kuwa tume rasmi ya uchunguzi inaonesha kuwa kitengo maalum cha polisi kiitwacho Berkut kilichobuniwa kukabiliana na vurumai kiliwauwa waandamanaji kadhaa katika uwanja wa maandamano mjini Kiev, mwezi Februari.

Amasema kikosi hicho maalum cha polisi kimevunjiliwa mbali.
Kaimu Waziri mkuu Arseniy Yatsenyuk ameiambia BBC kuwa rais aliyengolewa madarakani Viktor Yanukovych na washirika wake ndio wahusika wakuu katika maafa hayo.

Zaidi ya watu 100 waliuwawa katika vurumai hilo.
Naye kiongozi mkuu wa upelelezi Nchini Ukrainne Valentyn Nalyvaychenko amesema kuwa idara ya upelelezi ya Urusi imetuma tani kadhaa za vilipuko na silaha hadi Ukraine.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top