Bunge kufichua siri za CIA
Kamati ya bunge la Marekani kuhusu ujasusi imeidhinisha kuwekwa wazi kwa sehemu mojawapo ya ripoti iliyoiita ya "ukatili" iliyoelezea jinsi maofisa wa shiriki la upelelezi la Marekani (CIA) wanavyowahoji wanaotuhumiwa wa ugaidi.

Lakini wanakamati wanasema kuwa itachukua muda kabla ya uchunguzi huo kuwekwa wazi kwa umma.

Baadhi ya ripoti iliyofichuliwa inasema kuwa idara ya CIA kila mara ilipotosha serikali kuhusiana na mtindo wake wa kuhoji washukiwa wa ugaidi wakati wa utawala wa Rais George W Bush.

CIA inapinga baadhi ya matokeo ya taarifa hiyo huku ikikiri kutenda matendo ambayo hayakuafikiana na sera za Marekani.
Stakabdhi za CIA Kufichuliwa kwa umma

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge la seneti Dianne Feinstein anasema matokeo ya kura iliyopigwa kuhusu ripoti hiyo inaonesha wabunge 11-3 waliipigia mswada huo kura huku akiita ni uchunguzi wa matokeo yanayotamausha.


"ripoti hiyo inaonyesha dhuluma inayoenda kinyume na hadhi ya taifa letu.


Hii inatia doa historia ya taifa letu na ambayo hairuhusiwi kamwe kufanyika. Hivi sivyo wamarekani wanavyofaa kufanya." Mwanasiasa huyo wa chama cha Democrat kutoka Carlifonia amesema.


Taarifa ya wanahabari inasema kuwa japo baadhi ya wanakamati wa chama cha Republican walikashifu ripoti hiyo kwa pamoja na wa Democrats, kulionyesha waziwazi mgawanyiko uliopo ndani ya wajumbe hao.


Matokeo ya uchunguzi huo uliyomo katika kijitabu cha ukurasa 500, yatatumwa kwa Rais Barack Obama ili kuchunguzwa, kutiwa saini, kisha kutolewa kwa umma.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top