Muda wa mwisho uliowekwa na Marekani wa mpango wa mashariki ya kati umemalizika.
Mchakato huo unaonekana kugonga mwamba.
Israeli na Palestina wamekataa kuendelea na mazungumzo zaidi.
Mazungumzo yao yalivunjika pale Israeli
ilipoukataa mpango wa amani baina ya makundi makuu mawili ya Wapalestina
wa kuunda serikali ya Umoja na hasira ya wapalestina kutokana na
ujenzi wa Israeli wa makazi mapya katika maeneo yanayokaliwa na watu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry
amekasirishwa na kitendo cha Israeli kuendelea kujenga maakazi ya
Wayahudi na Palestina kupendelea kuunda serikali ya umoja na kundi la
Hamas.
Hata hivyo hajakubali kushindwa anatumia maneno kama ''kusitishwa kwa muda kwa harakati za kutafuta amani''.
Kuna uwezekano kuwa huenda Marekani itafuatilia
kwa karibu yanayoendelea huku ikishinikiza kurejelewa kwa mchakato wa
kutafuta Amani.
Hatahivyo baadhi ya washirika wa Marekani katika mazungumzo hayo wanamasema kuwa muda wa kuleta Amani umekwisha.
Viongozi wa nchi za Ulaya na matiafa ya Kiarabu
wameunga mkono juhudi za John Kerry katika kujaribu kulitafutia suluhu
tatizo la Israil na Palestina na kushikilia msimamo kwamba Marekani ndio
taifa pekee lenye uwezo mkubwa wa kufanikisha mchakato huo.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment