Shirika la Fedha Duniani, IMF, limesema Urusi kwa
sasa imeingia katika kipindi cha "mdororo wa uchumi" kutokana na hasara
iliyosababishwa na mgogoro wa Ukraine.
Shirika hilo, ambalo limeshusha makadirio yake
ya kukua kwa uchumi wa Urusi, limesema nchi hiyo mwaka huu itapoteza
dola bilioni 100.
Mkuu wa ujumbe wa IMF nchini Urusi,
Antonio Spilimbergo, amesema vikwazo vya kimataifa vinaharibu uchumi wa
Urusi na kutishia uwekezaji.
Uchumi wa Urusi, ulisinyaa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.
Lakini Bwana Spilimbergo amesema anatarajia hali hiyo kuendelea.
"Kama unaelewa mdororo wa robo mbili za kushuka
kwa uchumi, basi ufahamu Urusi inakabiliwa na mdororo kwa sasa," amesema
Bwana Spilimbergo.
Shirika la IMF limeshusha makadirio yake ya
kukua kwa uchumi wa Urusi mwaka 2014 kutoka asilimia 1.3% hadi asilimia
0.2% na kusema kwamba Shirika hilo linatarajia uchumi wa Urusi kukua kwa
asilimia 1% tu mwaka unaofuata.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment