
Msanii mmoja nchini Ufaransa
anajiandaa kulala ndani ya tumbo la Dubu wake aliyewindwa na kuhifadhiwa
katika makavazi ya wanyamapori mjini Paris.
Uamuzi wake huu umetajwa kama kuchagua kati ya maisha ya binadamu na wanyama.
Msanii huyo mfaransa anaanza
maonyesho yake ya kiusanii ambayo yametajwa kuwa ya kipekee na ambayo
yatashuhudia akilala ndani ya mnyama huyo kwa siku 13.
Abraham Poincheval aliyezaliwa mwaka 1972 kwa
mara ya kwanza alifanya maonyesho hayo yanayojulikana kama -kuishi ndani
ya ngozi ya Dubu- katika kituo cha maeonyeso ya usanii mjini Digne
mwaka jana.
Sasa anajiandaa kurejelea onyesho hilo katika
makavazi mjini Paris ambako atasalia ndani ya tumbo la Dubu huyo ambaye
ni mnyama halisi isipokuwa tu amekaushwa na kuhifadhiwa katika makavazi
hiyo.

Abraham Poincheval akichunguza ndani ya Dubu wake katika makavazi ya wanyama waliowindwa na kuhifadhiwa.
Poincheval aliwahi kuishi ndani ya shimo chini ya maktaba mjini Marseilles Oktoba mwaka 2012.
Inaarifiwa mwanaume huyo ni mjuzi wa maonyesho ya usanii yenye kutumia mbinu hatari.
Poincheval atakula, kulala na hata kwenda haja akiwa ndani ya tumbo la Dubu huyo, huku akinaswa na kamera mbili.

Abraham Poincheval akipanda ndani ya Dubu wake kabla ya kuonyesha atakavyojifungia ndani.
Duru zinasema kuwa kilichompa Poincheval motisha
ya kuishi ndani ya mzoga wa mnyama huyo, ni mizoga ya wanyamapori
aliyokuwa anakutana nayo mara kwa mara nchini Ufaransa.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment