Uvutaji wa sigara umeleta maafa, baada ya mtu mmoja kukatwa mkono na kuuawa na mwenzake wakati wakigombea sigara.
Katika tukio hilo lililotokea Korogwe, Jumapili
iliyopita, Februari 2, mnamo saa nne asubuhi, Idi Mkono, mwenye umri wa
miaka 30 alimkata mkono Ramadhani Gudelo (35) na kumuua baada ya kutokea
ugomvi uliohusu sigara.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine
Massawe alisema kuwa Polisi Tanga wako katika msako mkali wa kumtia
nguvuni Iddi Mkono (30) kwa tuhuma za mauaji.
Kamanda Massawe ameitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, badala yake wafuate taratibu na sheria zilizopo.
Wakati huo huo, watu wawili wanashikiliwa na
polisi, mkoani hapa kwa tuhuma za kukamatwa na lita 147 za pombe haramu
ya gongo maeneo ya Handeni, mkoani Tanga.
Kamanda Massawe alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa watuhumiwa hao lilitokea Februari 2 mwaka huu saa 5:30 asubuhi.
Massawe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hussen Muhadu (48), pamoja na Ramadhani Ugarawe (40), wote wakazi wa Chanika Handeni.
Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Aidha Kamanda Massawe aliwaonya wananchi kuchukua
tahadhari na matendo ya uhalifu wa aina yoyote ambao unaweza kusababisha
kuvunja sheria, huku akionya kuwa kwa yeyote atakayekiuka sheria
zilizowekwa atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu
zilizowekwa.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment