
Wanawake wa kabila la waturkana huko nchini Kenya
Serikali ya Kenya imeripotiwa kutuma maafisa wa
polisi kuongeza ulinzi katika kijiji cha Lorokon kaskaskani mwa count ya
Turkana mahali ambapo watu wenye silaha walikuwa wamezingira vituo
vitatu vya polisi ambao pia inasemekana wamewataka wanavijiji.
Gavana wa eneo hilo Josephat Nanok amelimbia
shirika la habari la Kenya KNA kuwa zaidi ya wanavijiji 900 wengi wao
wakiwa ni wanawake na watoto walizingirwa na watu hao wenye silaha na
kushindwa kutoka kwenda kutafuta chakula na maji.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema ugomvi wa
mpaka baina ya jamii mbili za makabila ya Waturkana na Wapotok ndio
chanzo cha tukio hilo.
Awali iliripotiwa kuwa watu wenye silaha kutoka jamii ya kabila la wapotok wamezingira kijiji cha Lorogon kwa siku nne.
Televisheni ya Kenya iliripoti mazungumzo ya
kutatua mgogoro huo kati ya makabila hayo yanayogombana yalitarajiwa
kufanyika siku ya jumapili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment