Wiki chache baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha
kutimuliwa kwa madai ya kukihujumu chama hiho, jana jioni Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda alitimuliwa katika kikao cha Kanda ya Ziwa Mashariki kwa madai ya usaliti.
Kikao hicho ambacho kilikuwa kinaendelea kufanyika mkoani
Shinyanga katika Hotel ya Karena, kinajumuisha wajumbe wa mikoa ya
Simiyu, Shinyanga na Mara inayounda Kanda ya ziwa Mashariki.
Hali ilianza kumbadilikia baada ya viongozi wa
kitaifa wakiongozwa na mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe,
kufika ukumbini hapo ambapo majira ya saa 1:00 jioni, mjumbe mmoja
alisimama na kutoa hoja kuwa kikao hicho hakiwezi kuendelea kujadili
masuala ya msingi ya chama ilihali kikiwa na watu ambao wanatoa taarifa
CCM.
Mjumbe huyo, alibainisha wazi kuwa mtu
anayemkusudia katika kikao hicho ni Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi
ya Chadema John Shibuda, ambaye alisema amekuwa akisimama katika
mikutano ya CCM na kuhutubia huku akijiita mwana Chadema.
Alieleza hivi karibuni, Mbunge huyo alikuwa katika
kikao cha CCM ambapo alisimama kuhutubia mbele ya Nape na kudai kua
vyama vya wapinzani havina kitu na kwamba CCM ndicho chama Tawala.
“Hatuwezi kuendelea na kikao hiki tukiwa tunajadili
masuala ya kwetu wakati tunaye mtu anayetupinga hadharani kwa mwenendo
wake na matendo yake bora, Shibuda huyu katika mkutano wa CCM Meatu
mbele ya Nape na Kinana, alisimama jukwaani na kuisifia CCM kuwa ndicho
chama makini na wapinzani ni watoaji matusi tu, hivyo napendekeza
atupishe kwa amani,” alikaririwa mjumbe huyo akimtaka Mbowe kumwondoa
Shibuda katika mkutano huo.
Kutoka na hoja hiyo wajumbe ndani ya mkutano huo
waliunga mkono na wote kutaka atolewe hali iliyomfanya Mwenyekiti Mbowe
kuwasihi wajumbe kumpa nafasi ya kujieleza kwa vile ni kiongozi na
kubainisha kwamba hakuja kufukuza mtu katika kikao hicho.
Baada ya hooja hiyo ya Mbowe wajumbe walitulia na
ndipo Mwenyekiti alipompa nafasi ya kujieleza na kudai kuwa CCM ni chama
tawala na kutoa misemo na mifano kadhaa hali ambayo ilizua kelele za
wajumbe wakimtaka kutoka nje na misemo yake.
Aidha katika utetezi wake Shibuda alisema kwamba
mtu mzima unapokuwa na shida yoyote unakwenda kwa Baba yako, CCM ni
chama Tawala hivyo yeye anakiona kama Baba yake hasa napokuwa na
matatizo Jimboni kwake.
Kauli hii ilionekana
kuwaudhi zaidi wajumbe wa kikao hicho na kuanza kumshambulia kwa maneno
hali ambayo ilimfanya Mbowe kuingilia kati na kuwataka wajumbe kupiga
kura iwapo wanakubaliana kuwa abaki katika kikao ama atoke. ambapo wajumbe
wengi wakawa upande wa atimuliwe huku kura 2 zikimtaka abaki
katika kikao.
Hivyo majira ya saa 1:23 jioni Mbowe alimwomba atoke nje
ya kikao hicho na kuheshimu kura za wajumbe hao na hoja hiyo kuishia
hapo na kikao kuelendea.
Via Mtandao-net
0 comments:
Post a Comment