UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
OFFICE OF
THE DEPUTY VICE-CHANCELLOR
(ADMINISTRATION)
P.O. BOX 35091 - DAR ES SALAAM – TANZANIA
Tel.: 022
2410500 - 8 Ext. 2003
022 2410394 - Direct Line
Fax: 022 2410718
Ref:
z1/18
|
|
Telegram: University of Dar es
Salaam
E-mail: dvc-pfa@admin.udsm.ac.tz
21 Juni, 2013
|
Wanajumuiya Wote
YAH: KUFUNGWA KWA SEHEMU YA BARABARA YA
KONTENA—KANISANI/MSIKITINI—CHANGANYIKENI
Uongozi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam unautaarifu umma kuwa kipande cha barabara kuanzia kumbi
za mihadhara ya Yombo 1&2 na Bweni Na. 6 hadi barabara ya Changanyikeni
kitafungwa kuanzia Jumapili tarehe 23 Juni 2013.
Barabara inayoanzia kituo
cha daladala cha Kontena hadi Bweni Na. 6 ilitengenezwa kwa ajili
ya matumizi ya ndani ya Chuo tu, ingawa kwa siku za karibuni matumizi ya
barabara hiyo yameongezeka kiasi cha kuhatarisha usalama wa wanafunzi na
wafanyakazi wanaotumia kumbi za mihadhara na ofisi zilizopo maeneo hayo.
Kwa hiyo, watu wote
waliozoea kutumia barabara hiyo kuelekea Changanyikeni kwa vyombo vya usafiri
vya moto, wanashauriwa kutumia barabara ya kawaida inayoanzia au kutokea karibu
na tawi la NBC.
Prof.
Y. D. Mgaya
NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO - UTAWALA
0 comments:
Post a Comment