Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela.
Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town,
Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya
rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo
kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa
akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa
wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani
kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa
kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa
karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza
jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana.
Chanzo: BBC-Swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment