Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka jana bungeni na kusema
Serikali inafahamu ukweli wa mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa
chama hicho jijini Arusha.
Chama hicho kimesema Serikali ilitumia kutokuwepo
kwao bungeni kupotosha wananchi kuhusu hali halisi juu ya mlipuko wa
bomu hilo uliotokea wakati chama hicho kikihitimisha kampeni zake za
uchaguzi mdogo wa udiwani katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha, Juni
15, mwaka huu.
Akizungumza kabla ya kuanza kuchangia muswada wa
sheria ya fedha ya mwaka 2013/2014, Waziri kivuli wa Nyumba, Ardhi na
Maendeleo ya Makazi wa Chadema, Halima Mdee alisema, “Kabla sijaanza
kuchangia Mheshimiwa Spika naomba nianze kwa kuwapa pole wakazi wote wa
Arusha kutokana na mlipuko wa bomu uliosababisha watu kupoteza maisha,
kwani tangu limetokea tukio hilo leo ndiyo nazungumza kwa mara ya
kwanza,”
“Tunazilaani kauli potofu zilizotolewa na Serikali
hapa bungeni, Serikali inajua nini kilichotokea Arusha na ilitumia
kutokuwepo kwetu kuupotosha umma,” alisema Mdee.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment